Thursday, May 2, 2013

MADIWANI nao WAPO

Mbeya. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, wameridhia kuanzishwa kwa Benki ya Wananchi, lakini wameiagiza halmashauri kuwaelimisha kwanza wananchi namna ya kupata mtaji wa uanzishwaji badala ya kutumia wazo la kuwakata Sh200 kutoka mauzo ya kahawa kwa kila kilo.
Akichangia hoja hiyo diwani kutoka Kata ya Bara, Weston Songa alisema madiwani hawana pingamizi na kuwapo kwa benki ya wananchi, bali wanashauri elimu kwanza ipite kwa wananchi ili wakilielewa waridhie mkakati wa kupata mchango ambao ndiyo utakuwa mtaji wa kuanzia.
Diwani kutoka Kata ya Isansa Emir Mzumbwe alisema wazo la awali la kuanzishwa kwa benki hiyo Julai litawezekana kutokana na kuwa muda huo ndiyo mazao yanauzwa
Mkurugenzi Mtendaji, Levisson Chilewa alisema wananchi walishakubali.
ewa benki hiyo ulianzia kwa kuuza wazo kwa wananchi ambalo lilikubaliwa na kwamba kinachotakiwa ni madiwani hao kukubali ili waweze kuanza kukusanya mtaji wa kuanzishia.

No comments:

Post a Comment