Thursday, May 23, 2013
KANISA NA MSIKITI:
NDUGU ZANGU WATANZANIA INATAKIWA KUJUWA YA KUWA JILA JICHO LITAFUMBA NA KILA PUMZI HITAKATA HIVYO BASI ATUNABUDI KUOMBA NA KUABUDU WAKRISTU KWA WAISLAMU AMINA.
MTWARA YAGEUKA KUWA IRAQ NA PALESTINA
Sasa umefika wakati wa kila Mtanzania kutambua kitu gani kinacho tokea Mkoani Mtwara kwasasa. Punde mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Bungeni kutangaza kuwa Gesi itatoka kwenda Dar es salaam kwanjia ya Mabomba. Mpaka sasa hari ya Mkoani Mtwara si nzuri, Baada ya tamko hilo wananchi wa Mkoani Mtwara wanaipinga vikari Kauli hiyo kwa kuandamana huku wakiimba nyimbo ya (HAITOKI) yaani wakimaanisha Gesi haipelekwi kokote. Huku fakifanya fujo kwa kuchoma magurudumu ya magari Barabarani. Siyo hayo tu bali mpaka sasa kunauharibifu wa mari na miundombinu likiwemo Daraja linalo unganisha Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa jirani (Daraja hilo maarufu kama Mikindani) Nje kidogo ya Mtwara Mjini. Ni hayo tu kwasasa mengi na mengineyo usikose kutembelea BLOG YETU.
Friday, May 10, 2013
Friday, May 3, 2013
ULIMBUKENI WA KIJANA HUYO NDIO HUU.
Kijana huyo baada ya kupata fedha ili akalipe Ada akaamua kuanza kupiga nazo picha. hizo ni ada akija kupata mwenyewe za kwake dunia nzima itamfahamu kuwa kapata fedha. kijana acha sifa za kijinga
DU! KWELI HII NDIO TANZANIA
maisha ya kulala double mpaka chuo, mmmmmmmmhhhhhhhh sijui tutafika kweli huko tunako kwenda maana kila kukicha afadhari ya jana. mungu tushike mkono .
Thursday, May 2, 2013
CCM wamgeuka RC Arusha: WADAI AMEMWONGEZEA UMAARUFU LEMA, CHADEMA
WADAI AMEMWONGEZEA UMAARUFU LEMA, CHADEMA
VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Wabunge hao waliliambia gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka za utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi CHADEMA.
“Mimi sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema aonekane shujaa.
“Leo tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda, lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema Lugola.
Mbunge mwingine ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema alichokifanya Mulongo ni sehemu ya tatizo kubwa la viongozi wa serikali kujihusisha na ukereketwa wa kisiasa.
“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa kuna kiongozi, tena hakumtaja jina, kwamba anapendwa kubebwa, alisema mwacheni abebwe. Alisema vile kuwazuia polisi kukabiliana na watu wanaopenda kumbeba kiongozi huyo.
“Mkuu wa Mkoa Arusha na wengine wanaokabiliana na wapinzani kwa nguvu kubwa bila sababu, hii inawaongezea umaarufu,” alisema mbunge huyo kutoka moja ya majimbo ya kanda ya kati.
Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya CCM ambaye pia hakutaka kutaja jina lake, alilaani jinsi mkuu wa mkoa huyo alivyojikoroga katika kushughulikia mzozo wa Chuo cha Uhasibu Arusha.
“Niliposoma ujumbe wa simu ya mkononi wa Lema ambao alidai umetoka kwa Mkuu wa Mkoa, nilishangaa sana. Sijui kwanini amefanya vile,” alisema kigogo huyo.
Aprili 24 mwaka huu, Mulongo aliliamuru Jeshi la Polisi mkoani Arusha kumkamata Lema kwa madai kuwa aliwachochea wanafunzi wa chuo hicho cha IAA kumzomea na kumrushia mawe.
Lema alizingirwa nyumbani kwake na maofisa wa polisi kitengo cha upelelezi na wale wa doria Ijumaa saa 5.30 usiku kisha kuchukuliwa hadi Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa na kuwekwa rumande siku tatu hadi Jumatatu wiki hii alipofikishwa mahakamani.
Hata hivyo, madai ya Mulongo kuwa Lema alichochea wanafuzni hao yanakinzana na ushahidi wa video unaoonesha kuwa mbunge huyo alitumia kila aina ya ushawishi kuwasihi wasiandamane kufuatia mwenzao Elly Kago (22) kuuawa na watu wasiojulikana jirani na chuo.
Mapema kabla ya kukamatwa, Lema aliitisha mkutano na waandishi wa habari akidai kutishiwa na Mulongo kupitia ujumbe wa maandishi wa simu.
“Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonyesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi,’’ ulisomeka ujumbe huo uliotumwa kupitia simu namba 0752 960276 ambayo Lema alidai ni ya Mulungo.
Atisha waandishi
Wakati CCM wakiendelea kumlalamikia Mulongo kwa hatua zake dhidi ya Lema, kiongozi huyo jana aliwageukia waandishi wa habari wa Arusha akiwataka wawe makini kipindi hiki, akidai kuwa nao wanatumika na wanasiasa.
Akihutubia katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi, alisema kuwa ikibainika wanatumika nao watafikishwa katika vyombo vya sheria.
“Mimi nilikuwa Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, hivi hivi wakawa hawanielewi na ikafika wakati wakanielewa kwani kuna miongoni mwao tulitaka kuwafikisha katika sheria, lakini tukayaacha kwa kuwa sisi ndio walezi,” alisema.
Mulongo aliongeza kuwa vitu ambavyo vinaandikwa si kweli kabisa, na kwamba wataendelea kufuatilia kwani baadhi ya waandishi wanashirikiana na wanasiasa kuwachafua viongozi wa serikali.
Alisema baadhi ya waandishi mkoani Arusha wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ushabiki wa kisiasa na kuandika mambo ambayo hawana uhakika nayo.
“Unapoingia katika mkakati wa kudhalilisha kiongozi wa serikali unakuwa umeiweka roho yako rehani, kuweni makini,” alisema.
Aidha alivionya vyama vya wafanyakazi mkoani Arusha kutoruhusu kutumiwa na watu kwa malengo ya kisiasa na pia waajiri waache kufanya kazi bila kufuata taratibu na sheria.
MADIWANI nao WAPO
Mbeya. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, wameridhia kuanzishwa kwa Benki ya Wananchi, lakini wameiagiza halmashauri kuwaelimisha kwanza wananchi namna ya kupata mtaji wa uanzishwaji badala ya kutumia wazo la kuwakata Sh200 kutoka mauzo ya kahawa kwa kila kilo.
Akichangia hoja hiyo diwani kutoka Kata ya Bara, Weston Songa alisema madiwani hawana pingamizi na kuwapo kwa benki ya wananchi, bali wanashauri elimu kwanza ipite kwa wananchi ili wakilielewa waridhie mkakati wa kupata mchango ambao ndiyo utakuwa mtaji wa kuanzia.
Diwani kutoka Kata ya Isansa Emir Mzumbwe alisema wazo la awali la kuanzishwa kwa benki hiyo Julai litawezekana kutokana na kuwa muda huo ndiyo mazao yanauzwa
Mkurugenzi Mtendaji, Levisson Chilewa alisema wananchi walishakubali.
ewa benki hiyo ulianzia kwa kuuza wazo kwa wananchi ambalo lilikubaliwa na kwamba kinachotakiwa ni madiwani hao kukubali ili waweze kuanza kukusanya mtaji wa kuanzishia.

MADEREVA KUITUNISHIA SERIKALI KIFUA.
Dar es Salaam. Madereva wa malori yanayofanya safari zake ndani na nje ya nchi wametangaza mgomo kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kusimamia mikataba ya ajira ambayo mpaka sasa hawajapata.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo ambapo mpaka sasa Serikali na waajiri wao wameshindwa kulitekeleza jambo ambalo limewafanya wawe vibarua wa kudumu
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rocket Matogoro alisema kuwa, mgomo huo utaanza Mei 10 mwaka huu ambapo madereva hao hawataendesha magari hayo mpaka suala hilo litakapotekelezwa. “Madereva wa malori tumeandaa mgomo ili kuishinikiza Serikali kusimamia mikataba yetu ya ajira ambayo mpaka sasa imekuwa hewa, jambo ambalo linatufanya waajiri watudharau,”alisema Matogoro.
Alisema kutokana na hali hiyo madereva hao siku hiyo hawataondoa magari katika maegesho mpaka suala hilo litakapomalizwa. Mbali na hilo,madereva hao wameitaka Serikali kujenga maegesho ya magari katika vituo ambavyo vimepangwa ili kuondoa usumbufu unaojitokeza sasa

HII NDIO TANZANIA NA MAISHA YETU NDO AYOOOOOOOOOOOOOO
HII INAONYESHA KUWA INCHI HII NA SERIKALI ILIYOPO MADALAKANI JINSI ILIVYO SHINDWA KUTOA UDUMA BORA KWA WANAINCHI WAKE. HAKI YA MAMA IKO WAPI ? KWELI MAISHA BORA KWAKILA MTANZANIA.
Membe kugombea urais mwaka 2015 iwapo...
1
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe,
amesema atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015, iwapo wananchi wataona anafaa
na kumtaka afanye hivyo.
Alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya mwandishi wa habari hii mjini hapa, baada ya kumalizika kwa kongamano la vyuo vya elimu ya juu mkoani hapa, lililofanyika katika ukumbi wa St. Dominic.
Membe aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alisema ingawa muda wa kufanya uamuzi kuhusu mwaka 2015 bado na chama hakijatoa utaratibu, lakini atasubiri ushauri wa Watanzania.
"Naomba kurudia, mimi nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza kugombea urais ...ila nasema hivi natarajia sana ushauri wa Watanzania.
“Iwapo Watanzania wataniona nafaa na kunitaka nigombee, nitapima mawazo yao na iwapo ni wananchi wengi watakaoniunga mkono kutaka nigombee, basi nitachukua fomu na kuijaza ili nigombee nafasi hiyo kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu," alisema Waziri Membe.
Maadili ya wabunge Membe alisema hali ya kisiasa nchini inakwenda vibaya kutokana na kila mtu kuzungumza mambo bila kujitathmini. Alisema mbaya zaidi hata baadhi ya wabunge wa CCM, nao wamekuwa si msaada kwa chama, kutokana na kuzungumza mambo dhidi ya Serikali na chama.
Membe alisema amepata kukaa bungeni kwa zaidi ya miaka 15 tangu Bunge la Spika Pius Msekwa, hadi sasa chini ya Spika Anne Makinda, ila anachokiona ni baadhi ya wabunge kukosa maadili na kuzungumza mambo bila kuzingatia kanuni za Bunge, jambo ambalo ni hatari zaidi.
Alisema Bunge linalotazamwa na Watanzania, ni lazima liwe la mfano wa kuigwa na lenye kuzingatia maadili katika kuzungumza, lakini sasa ndio maana Bunge linaendelea kupoteza mwelekeo.
"Bunge linapoteza mwelekeo kutokana na mawazo ya baadhi ya wabunge wanaofikiri wakisema ovyo na kutumia lugha kali katika kuzungumza, wao ndio wanaonekana ni wabunge bora kitu ambacho hakipo.
“Mbunge ni pamoja na kujiheshimu na kutumia lugha nzuri katika kuwakilisha wapiga kura wako bungeni," alisema.
Membe alisema kutotumia busara katika kujadili mambo bungeni, si ubunge mzuri na bora watambue wazi kuwa wananchi wao wanawatazama na hukumu yao itatolewa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kama hicho wanachokifanya, ni kuwakilisha wananchi au kujiwakilisha.
"Nawaomba wabunge wawe wazalendo, wawakilishe wananchi waliowatuma badala ya kuligeuza Bunge kama sehemu ya kuonesha ujuzi wa kuzungumza ovyo.
“Nasema tuogope wananchi, mwaka 2015 watatoa adhabu kwa kila mbunge na kwa sasa wananchi wanasikiliza na kutazama ila muda ukifika watakuacha," alisema.
Alisema wabunge wengi ni vijana na wanafikiri kusema vibaya juu ya CCM ndio ubunge bora, ila watu watafanya uchunguzi wa kutembelea jimbo la mbunge husika na kuangalia amefanya nini katika jimbo lake na watampima kwa kazi aliyofanya na si ukali bungeni.
Alisifu baadhi ya wabunge wa CCM, kwamba wamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika majimbo yao, kwa chama na Serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete, kwa kusukuma mbele maendeleo ya Taifa, ila baadhi yao wapo kwa ajili ya kuonesha uwezo wa kusema ovyo.

Kimenuka: lady jay Dee afunguka, Atoa wosia wake siku akifa
WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA
NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge. Nilivumilia fitna mannikin ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

Subscribe to:
Posts (Atom)