Monday, July 15, 2013

SHEKHE WA WILAYA AMWAGIWA TINDI KALI:

Sheikh Makamba anayekaimu nafasi hiyo alikutwa na hayo kati ya Saa 4:00 hadi 5:00 usiku wa kuamkia juzi akitoka kusali Tarawei na alilazwa wodi namba nne katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu.

Vitendo kama hivi havitakiwi kabisa ktika jamii zetu,
havito tuzidishia isipokuwa chuki zaidi na mfarakano baina yetu.

Lakini hebu tujiulize:Hivi kitendo kama hiki kingetokea kwa Mchungaji au Padri hali ingekuwaje?
Ni nani angekuwa ananyooshewa vidole hivi sasa?

Twamuomba Allah amponye imamu huyu na awaponye wagonjwa wote.
Aamiiiin

Sunday, July 7, 2013

TAREHE 7 MWEZI WA 7

Zitto ashindwa kutokea kwenye pambano lake na Ray. Atoa udhuru wa kutokuwepo. Soma hapa

  • Zitto ashindwa kutokea kwenye pambano lake na Ray. Atoa udhuru wa kutokuwepo. Soma hapa 1
Mheshimiwa Zitto kabwe ameshindwa kufika leo uwanja wa taifa kupambana na mwigizaji Vicenti kigosi katika pambano lao la ngumi lililopangwa kufanyika usiku wa leo kutokana na majukumu ya kikazi. Akitoa udhuru huo kupitia ukurasa wake wa facebook hichi ndicho alichokisema.
"Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji. 

TAMASHA LA MATUMAINI
Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. 
Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.
Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.
Nawaomba muiombee amani nchi yetu na msimamie haki kwa wananchi wote bila kubagua dini zao, rangi zao, hali yao kimaisha na ufuasi wa vyama vya siasa. Mwaka huu tumeshuhudia matukio ambayo yanatikisa msingi wa Taifa letu – Umoja.
 Hivi sasa msingi wetu una nyufa ambazo kwa kweli hatujajua bado nini kinacholeteleza mambo haya kama kulipua makanisa, kulipua mikutano ya vyama vya siasa na kuua viongozi wa dini. 
Matukio haya yanatuelekeza kuwa makini sana na kauli zetu kwani baadala ya kuunganisha wananchi tunawezajikuta tunawagawa zaidi Watanzania na hivyo kuwa na mzunguko wa machafuko (vicious circle of violence). 
Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa na wananchi kuepuka kabisa kuanza kurushiana maneno na lawama kuhusu matukio haya, kwani inawezekana lawama na maneno yetu yakawa yanampa nguvu adui wetu ambayo hatujamjua bado.
Napenda niwakumbushe kwamba ni rahisi sana kusambaza chuki na ni vigumu sana kuondoa chuki miongoni mwa wananchi.
Viongozi hatari kama Hitler walitumia sana mbinu ya kueneza chuki dhidi ya jamii ya Jews na matokeo yake yalikuwa ni vita vikuu vya pili vya dunia na zaidi ya watu milioni 6 wasio na hatia kupoteza maisha.
 Sisi sote tuna jukumu moja la kuhakikisha tunajenga Taifa lenye kujali HAKI na lenye mshikamano mkubwa miongoni mwa raia. Kwa nia hii tu ndio tutaweza kuwa na Taifa imara lenye heshima mbele ya mataifa mengine duniani. Ni kwa njia hiyo tu ndio tutaweza kutokomeza umasikini uliokithiri mijini na vijijini hapa nchini kwa kuongeza uzalishaji na kupanua ajira. Ikumbukwe bila HAKI hakuna AMANI na bila UWAJIBIKAJI hakuna UTULIVU.
Tukiegemea siasa za CHUKI. Tukashindwa kuwa na mahusiano ya kawaida miongoni mwa viongozi kuhusu masuala ya msingi ya nchi. Tukashindwa kujadiliana kwa hoja kuhusu sera zetu. Tutapata viongozi aina ya Hitler nchini mwetu. Wote tukatae. Sisi ni Watanzania. Muwe na Tamasha jema la Matumaini."

Zitto Kabwe

SIJUWI NISEME NN

SINACHA KUONGEA JUU YA KIJANA HUYU ANAYEJITAMBUA NA ANAJUWA NN ANAFANYA KWA WAKATI


MWANACHUO HARAANI VIKALI ALICHOFANYIWA NA WANACHO WENZIE HOSTL

Vitendo  vya  wanafunzi  kupigana  exile( kumpisha room ili angonoke na mpenzi wake)   vimekuwa  vikishika  kasi  ya  ajabu  katika  hosteli  za  wanafunzi  wa  vyuo  vikuu  mbalimbali ambao  kwao  limekuwa  ni  jambo  la  kawaida...!!
Hali  imekuwa  ni tofauti  kidogo  kwa  mwanafunzi  wa  chuo kimoja  hapa  nchini  ambaye  yuko  mwaka  wa  kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.

Akiongea  na  mtandao  huu  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina , mwanafunzi  huyo  amefunguka  na kudai  kuwa  Exile  imemuathiri  sana  kisaikolojia.Imemfanya  aishi  kama  mtumwa  huku  taaluma  yake  ikiyumba  kwa  kasi.
Hili  ni   simulizi  la  mwanafunzi  huyo:
 
"Maisha ya shule yana changamoto  nyingi sana.Kwa  mtu  yeyote  ambaye  ni  mcha  mungu  ni  lazima  itamuwia  vigumu  sana  kukabiliana  na  hali hii.
"Nasema  hivi  kwa  sababu  ndani  ya  hosteli  huwa  tunaishi  watu   tofauti  wenye malezi  tofauti.Kasheshe  ni  kwetu  sisi  first  year...
"Mazingira  kwetu  ni  mageni  na  ndani  ya  hosteli  tunaishi  na  mabraza  wa  miaka  ya  juu  wenye  wapenzi  wao  hapo hapo chuoni ambao  huwaleta  vyumbani   na  wakati mwngine  hulala  nao.
"Wanapokuja  na  wapenzi  wao  vyumbani  ni  lazima  uwapishe  wafanye  mambo  yao.Na  ukiwapisha  maana  yake  utoke  kwa  zaidi  ya  masaa  matatu  mpaka   matano
"Ndani  ya  chumba  changu  tulikuwa  tunaishi  watatu, mmoja  mwaka  wa  pili, mwingine  wa  tatu  na  mimi  mwaka wa kwanza.Wote  hao  walikuwa  na  wapenzi  wao  hapo hapo  chuoni.
"Siku  zote  za  wikiendi  walikuwa  wamezigawana.Mmmoja  ilikuwa  ni  jumamosi  na  mwingine  jumapili.Yaani  kwa  kifupi  ni  kwamba  sikuwa  na  uhuru wa  kukaa  chumbani   siku za wikiendi  na  wakati  mwingine  hata  siku  za  wiki.
"Nimeamua  niwe  muwazi  maana hali  hii  imekuwa  ni  kero  kwangu   na  imekuwa  ikiniathiri  sana  kisaikilojia  na  kusababisha  taaluma  yangu  iyumbe  nikilinganisha  na  nilipokuwa  naanza.
"Naomba  nitoe  ombi  kwa  wanafunzi wenzangu.Sote  tuko  vyuoni  kutafuta  maisha  na  zile  hosteli  tunazilipia  kwa  gharama  sawa.Kwa  nini  umsumbue  mwenzako  wakati  gesti  zipo?..Yangu  ni  hayo  tu"